HISTORIA
Mimi Nilizaliwa mnamo mwaka 1990 katika kijiji cha Msowero,
wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro.
Mnamo ALHAJI MEJA HASAN
mwaka 1996 nilihamia Zanzibar
na kuishi huko na kujiunga na dini ya Kiisilamu na kupata elimu ya msingi mnamo
mwaka 1997 hadi mwaka 2003. Nilihitimu kidato cha nne mwaka 2007 nikiwa
hukohuko Unguja.
Baada ya hapo nilijiunga na kikosi cha KZ cha ulinzi na
usalama Zanzibar
mwaka 2009 hadi 2010 May ndipo nilihitimu.
Baada ya hapo nilisoma masomo ya Kiitaliano na Kiingereza
kwa mudawa miezi 9.
Niliajiriwa katika Bank ya NCCT Zanzibar ambayo inabadilisha
fedha za kigeni za kimataifa.
Nilianza kazi 2011 hadi 2015 ambapo mkataba wangu wa kufanya
kazi miaka 10 ulikwisha.
- KABLA YA KUOKOKA
Nilipitia mambo magumu katika maisha yangu ambayo yalinusuru/
gharimu/ hatarisha maisha yangu.
Siku moja kuna wageni walitoka Mataifa mbalimbali duniani,
na kati ya hao wageni mmoja anasadikika kwamba inaweza ikawa alitega bomu
karibu na Bank.
Sisi kama maaskari hatukujua
lolote. Wakati tunalinda nilisikia sauti ya Mungu ikisema nami kwamba niondoke
mahali hapo na kusogea mbali kidogo, bila kujua sababu niliitii ile sauti na
ndipo bomu lilipolipuka na kuwalipukia wenzangu watatu na kupoteza maisha yao na mimi kunusurika.
Baada ya siku sita kupita niliacha kazi mnamo tarehe
07/11/2015 kabla hata ya mkataba wangu kuisha ambapo pia ilinigharimu kwa
kampuni.
Kabla ya kuokoka nilidumu duniani kwa vile nilikuwa na pesa
ambazo hazikunisaidia baadaye.
Siku mija niliota ndoto na nikaoneshwa huku kuna maji na
huku kuna moto. Nikaambiwa na Malaika chagua unakotaka, nikabaki lalia niende
wapi! Ndoto hiyo moja ilijirudia kwa
muda wa siku sita na ndipo nikachukua jukumu la kuacha kazi.
Nikaona hela sio bora japo ni bora, nikaamua kumfuata Mungu.
Maisha yangu nilikula mirungi, nilivuta bangi na kunywa kila aina ya kilevi ili
niwe fiti katika kazi yangu ambayo ilinilazimu.
- HATUA ZA KUOKOKA NA KUMFUATA BWANA NA MWOKOZI YESU KRISTO
Baada ya kuacha kazi nilimtafuta Mchungaji wa kiroho wa
kanisa la Kipentekoste ambaye Mungu alisema nami, baada ya mafundisho mengi ya
neno la Mungu alinitubisha sala ya toba na kuwa mkristo mwaminifu wa kanisa la
Kipentekoste mwanzoni mwa mwezi Desemba 2015. Kupitia huyo mchungaji ikawa ni
ukombozi mkubwa kwangu na mwanzo wa maisha mapya ndani ya wokovu.
Hadi
leo tarehe 07/01/2016 ninaendelea na Yesu wangu vizuri na siku ya Jumapili wiki
hii tarehe 10/01/2016 nitabatizwa ubatizo wa Yesu Kristo wa maji mengi ili
kutimiliza au kutimiza haki yote. Kwa kupata zaidi mafundisho ya ubatizo fungua
kwa biblianenohai@gmail.com
au click/ bofya hapo mbele UBATIZO
WA MAJI MENGI.
Nilikuwa
mwislamu tangu mwaka 1999 hadi mwaka 2015. Nimetumikia uislamu kwa muda wa
miaka 16. Kwa muda wote niliotumikia uislamu nilikuja kugundua nilipotea na
kuamua kumpa Yesu Kristo maisha yangu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu.
Kwa
sasa naishi maisha ya amani ndani ya Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wa maisha
yangu.
Bila
kokoka na kumpa Yesu maisha yako Mbinguni hutakwenda wewe ndugu yangu ambaye
bado haujaokoka. Yesu alikufa na kufufuka na sas yupo hai. Wengine wote
walikufa na mifupa yao
ipo kaburini hadi leo. Asanteni.
Jina
langu niliitwa Alhakim Meja Hasan. Na kitambulisho changu cha kazi ni
ID.EL/GUARD/no: Z.11036, Mwewe Security Company Ltd, PO Box 1203, Zanzibar,
Mobile +255 777 421159/ 0786111957, Email mwewesc@gmail.com
, position: Security Guard.
NINGEPENDA
VIJANA WENZANGU WA KI-AFRIKA NA TANZANIA MUWEZE KUSOMA USHUHUDA WANGU, MAANA NI USHUHUDA MKUBWA WA KUMTUMIKIA
MUNGU KULIKO KUTUMIKIA PESA.
Ukimtumikia
Mungu siku za maisha yako zitaongezwa kwa vile ni mpango wa Mungu. Ee ndugu
yangu, Rafiki, jamaa na Mtanzania mwenzangu badilika kupitia ushuhuda wangu
ulio na mapito makubwa sana.
(JESUS IS MY SAVIOUR/ YESU KRISTO NI MWOKOZI WANGU)
Baada
ya kuokoka nampenda Mungu sana,
kwa sababu ameniponya kutoka mautini.Ewe kijana mwenzangu chukua uamuzi
sasa wa kuokokoa yaani kuongozwa sala ya
toba na kubatizwa maji mengi. Jina lako litafutwa katika kitabu cha hukumu na
kuandikwa katika kitabu cha uzima wa milele.
Kama
hujaokoka jina lako lipo katika kitabu cha hukumu na siku mija utaja kulia sana utakapokwenda katika
moto wa milele, huko utajalia na kusaga meno
Badilikeni
kupitia ushuhuda wangu. Soma Matendo 4:1-3. Yesu ni
njia ya uzima (Jesus is way of life)
Jifunze
kupitia maono yangu na chukua hatua ya kubadilika ili ili upate kuokolewa ewe
Baba, mama, dada, kaka na ndugu yangu, bibi na babu yangu. Utapata uponyaji wa
kiroho na kimwili, kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi au maji tele.
Baada
ya hapo utapata mahusiano mazuri na Mungu na kila jambo utakaloliomba litatimia
au kutimizwa.
Ewe
ndugu yangu usidanganyike na ubatizo wa maji kidogo hatakusaidia. Kubatizwa
maana yake ni kuzikwa utu wa kale. Ubatizo wa maji kidogo maana yake umezika
kichwa tu na kiwilili chako kipo nje kwa shetani.
Epukeni
madhara ya uongo tafuteni kanisa la kiroho.
Makanisa yapo mengi TAG, FPCT, EAG(T), PENTEKOSTE NK na utapata thawabu.
Makanisa yapo mengi TAG, FPCT, EAG(T), PENTEKOSTE NK na utapata thawabu.
Kwa
mungu ilitangazwa manabii wengi watakuja kwa jina langu, hivyo tuwe makini sana.
Yesu
alibatizwa ubatizo wa maji tele katika mto wa jordani. Ubatizo wa maji mengi
maana yake unakufa pamoja na Kristo Yesu na unafufuka pamoja naye kwenye uzima
wa milele.
Asante
Mungu kwa uwepo wako na kunisaidia kutoa ushuhuda wangu na kuushuhudia kwa
mataifa. Neno lako linapita kila neno.
Neno
la Mungu likuinue kiroho na kukubariki.
Mungu
ubariki ushuhuda wangu huu na ukutumikie siku zote kwa wote watakaousoma
wabarikiwe na kubadili maisha yao
milele na hata milele Amina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni